Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 8:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 kwa khiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba pamoja na kutusihi tuipokee neema hii, na kushirikiana nao huku kuwakhudumia watakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 walitusihi sana wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 walitusihi sana wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 walitusihi sana wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 wakitusihi kwa bidii wapewe fursa ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 wakitusihi kwa bidii wapewe fursa ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watakatifu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 8:4
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake.


Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.


Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na killa mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.


Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi.


Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha.


Baada ya miaka mingi nalifika niwaletee watu wa taifa langu sadaka na matoleo.


niokolewe nao waasio katika Yahudi, na tena khuduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemi ipate kibali kwa watakatifu,


KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo.


Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu),


KWA khabari za kuwakhudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia.


illa neno moja walitutakia, tuwakumbuke maskini; na neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo