Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 8:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa shidda nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa unyofu wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ingawa walikuwa na majaribu makali, furaha yao kubwa na umaskini wao mkuu zilifurika kwa ukarimu mwingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Pamoja na majaribu makali na taabu walizopata, furaha waliyokuwa nayo ilikuwa kubwa, ingawa walikuwa maskini kupindukia, kwa upande wao walifurika kwa wingi wa ukarimu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 8:2
20 Marejeleo ya Msalaba  

Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu nipendavyo? Au jicho lako ni ovn kwa sababu ya kuwa mimi mwema?


mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukarimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha.


Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba?


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Maana naliandika kwa sababu hii pia, illi nipate bayana kwenu kwamba m wenye kutii katika mambo yote.


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.


kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.


Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,


Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo