Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 8:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nias katika jambo la neema hii inayokhudumiwa nasi, illi Bwana atukuzwe, ikadhihirike ya kuwa mioyo yenu ilikuwa tayari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makundi ya waumini ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana Isa mwenyewe, na ili kuonesha hisani yetu kuwasaidia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makundi ya waumini ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana Isa mwenyewe, na ili kuonyesha hisani yetu kuwasaidia.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 8:19
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


bassi tumeona vema tukiwa tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paolo,


Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo.


Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.


Wala si hivyo tu, illa na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambae kwa yeye tuliupokea upatanisho.


Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu,


Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe.


Lakini sasa mkatimize kule kutenda nako, illi kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mwe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.


Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.


Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu katika khabari ya karama hii inayokhudumiwa nasi;


Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.


Na Mungu aweza kuwajaza killa neema kwa wingi, illl ninyi, mkiwa na riziki za killa namna siku zote, mpate kuzidi sana katika killa tendo jema;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo