Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 8:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, wapata mwaka, licha ya kutenda hivi, hatta kutaka pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: Inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Nyinyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: Inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Nyinyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Nyinyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu katika jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu juu ya jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 8:10
18 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake.


Ninyi hamjui neno lo lote, wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu hawa, wala lisiangamie taifa zima.


Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu.


Na Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi shauri kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.


Vitu vyote ni halali kwangu; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali kwangu; hali si vitu vyote vijengavyo.


Siku ya kwanza ya juma killa mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; changizo zisifanyike hapo nitakapokuja:


Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.


Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana.


Lakini yu kheri zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi; nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho ya Bwana.


SINA buddi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia njozi na mafunuo ya Bwana.


hatta tukamwonya Tito kuwatimilizieni neema hii kama vile alivyoianza.


Sineni illi kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu.


Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo