Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 7:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Wala si kwa kuwapo kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu khabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hatta nikazidi kufurahi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Si tu kwa kule kuja kwake Tito, bali pia kwa sababu ya moyo mliompa nyinyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamani kuniona, jinsi mlivyo na huzuni, na mnavyotaka kunitetea. Jambo hili linanifurahisha sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Si tu kwa kule kuja kwake Tito, bali pia kwa sababu ya moyo mliompa nyinyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamani kuniona, jinsi mlivyo na huzuni, na mnavyotaka kunitetea. Jambo hili linanifurahisha sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Si tu kwa kule kuja kwake Tito, bali pia kwa sababu ya moyo mliompa nyinyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamani kuniona, jinsi mlivyo na huzuni, na mnavyotaka kunitetea. Jambo hili linanifurahisha sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini si kule kuja kwa Tito tu, bali pia kwa faraja mliyompa. Alitueleza jinsi mlivyonionea shauku, huzuni yenu kubwa na juhudi yenu kwa ajili yangu, ili furaha yangu ipate kuwa kubwa kuliko wakati wowote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Lakini si kule kuja kwa Tito tu, bali pia kwa faraja mliyompa. Alitueleza jinsi mlivyonionea shauku, huzuni yenu kubwa na juhudi yenu kwa ajili yangu, ili kwamba furaha yangu ipate kuwa kubwa kuliko wakati wowote.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 7:7
34 Marejeleo ya Msalaba  

Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.


Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika.


Nae kwa kuwa alikuwa na huzuni sana, akazidi kuomba kwa bidii. Hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka hatta inchi.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.


Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo.


vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.


atufarijiye katika shidda zetu zote illi tupate kuwafariji wale walio katika shidda za namna zote, kwa faraja tunazofarijiwa na Mungu.


Maana naliandika kwa sababu hii pia, illi nipate bayana kwenu kwamba m wenye kutii katika mambo yote.


Maana na sisi katika hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa vazi jingine, yaani kao letu litokalo mbinguni;


Illakini Mungu, mwenje kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuwapo kwake Tito.


Maana ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule sijuti, ijapokuwa nalijuta; maana naona ya kwamba waraka ule nliwahuzunisha, ijapokuwa ni kwa kitambo.


Lakini Mungu ashukuriwe atiae bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.


kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.


Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.


Lakini Timotheo alipotujia siku hizi kutoka kwenu, akatuletea khabari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote: mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi ninyi;


Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana.


KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.


Eliya alikuwa mwana Adamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye: na mvua haikunya juu ya inchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.


Nalifurahi mno kwa kuwa naliwaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.


Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo