Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 7:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Nina ujasiri mwingi kwemi; kujisifu kwangu kwa ajili yenu ni kwingi. Nimejawa na faraja, katika mateso yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Nina ujasiri mwingi kwa ajili yenu; naona fahari juu yenu. Nimejawa na faraja. Nina furaha kupita kiasi katika mateso yetu yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Mara nyingi najivuna kwa ajili yenu; naona fahari juu yenu. Nimejawa na faraja. Nina furaha kupita kiasi katika mateso yetu yote.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 7:4
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu,


Namshukuru Mungu wangu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;


vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.


atufarijiye katika shidda zetu zote illi tupate kuwafariji wale walio katika shidda za namna zote, kwa faraja tunazofarijiwa na Mungu.


Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga ninyi wala si kuwaangusha), sitatahayarika;


Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Illakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), na mimi niuao ujasiri.


Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.


Bassi, kwa kuwa tuna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;


Kwa maana, ikiwa nimejisifu kwake kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; hali, kama tulivyowaambieni mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.


Bassi waonyesheni mbele ya makanisa bayana ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.


Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.


kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.


kujisifu kwenu kupate kuzidi katika Kristo Yesu kwa ajili yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi nyote tena.


Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


Hatta sisi wenyewe twajisifu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya uvumilivu wenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na mateso mnayoyavumilia;


Maana tuna furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu lmeburudishwa nawe, ndugu.


Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo