Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 7:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu, hatukumharibu mtu, hatukumkalamkia mtu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Tupatieni nafasi mioyoni mwenu. Hatujamkosea mtu yeyote, wala hatujampotosha mtu yeyote, wala hatujamdhulumu mtu yeyote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Tupatieni nafasi mioyoni mwenu. Hatujamkosea mtu yeyote, hatujampotosha mtu yeyote, wala hatujamdhulumu mtu yeyote.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 7:2
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu.


Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma.


Msihame nyumba kwa nyumba. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisheni, vileni vitu vile viwekwavyo mbele yenu.


Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Nasema tena mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; mimi nami nipate kujisifu kidogo.


Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


Mpokeeni, bassi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.


Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.


Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;


niliyemtuma kwako, nawe umkubali, maana ni moyo wangu;


Bassi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi.


Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo