Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 7:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na khofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa killa njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: Nyinyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Nyinyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: Nyinyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Nyinyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: nyinyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Nyinyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Tazameni jinsi huzuni hii ya kiungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Tazameni jinsi huzuni hii ya kimungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 7:11
54 Marejeleo ya Msalaba  

Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:


Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako umenila.


Paolo alipokuwa akiwangojea katika Athene akaona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.


Marra haba. Yalikatiwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune bali uogope;


Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu.


Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)


illi kusiwe fitina katika mwili, hali viungo vitunzane.


Bali hao walio nje Mungu atawahukumu. Mwondoeni mtu yule mbaya, asikae kwenu.


Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo.


Na namwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, bali ninyi mfanye lililo jema, tujapokuwa sisi kama waliokataliwa.


Yamtosha mtu wa jinsi hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi;


bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Wala si kwa kuwapo kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu khabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hatta nikazidi kufurahi.


Sasa nafurahi, si kwa sababu ya kuhuzunishwa ninyi, bali kwa sababu mlihuzunishwa hatta mkatuhu. Maana mlihuzunishwa mmele za Mungu, msipate khasara kwa tendo letu katika neno lo lote.


Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.


Mwe na ghadhabu, wala msifanye dhambi; jua lisichiwe na uchugu wenu bado kukutokeni;


Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;


Bassi, wapendwa, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo, bali sasa zaidi mimi nisipokuwapo, utimizeni wokofu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka;


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


Wale watendao dhambi, uwakemee mbele ya watu wote, illi na wengine waogope.


Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.


Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.


BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni;


kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;


bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili.


Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo