Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 7:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Maana huzuni iliyo mbele za Mungu hufanyiza toba iletayo wokofu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanyiza mauti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kwa maana huzuni ya kiungu huleta toba iletayo wokovu, wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kwa maana huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 7:10
32 Marejeleo ya Msalaba  

Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.


Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.


Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:


nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.


Sasa nafurahi, si kwa sababu ya kuhuzunishwa ninyi, bali kwa sababu mlihuzunishwa hatta mkatuhu. Maana mlihuzunishwa mmele za Mungu, msipate khasara kwa tendo letu katika neno lo lote.


Maana mwajua ya kuwa hatta alipotaka baadae kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo