Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 6:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu; kwa silaha za haki mkononi wa kuume na mkononi wa kushoto;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 6:7
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.


Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.


bali kwao waitwao, Wayahudi na Wayunani pia, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


Kwa maana, ikiwa nimejisifu kwake kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; hali, kama tulivyowaambieni mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.


katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake,


Bassi, kwake yeye awezae kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuombayo au tuwazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu,


mkiwa mwalimsikia mkafundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli katika Yesu;


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu.


Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.


Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo