Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 6:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema: “Nitafanya makao yangu kwao, na kuishi kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema: “Nitafanya makao yangu kwao, na kuishi kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema: “Nitafanya makao yangu kwao, na kuishi kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mwenyezi Mungu aliye hai. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 6:16
60 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


Akawaambia mithali, Hakima apasuae kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu: ikiwa atia aipasua ile mpya, na kile kiraka cha nguo mpya hakilingani na lile vazi kuukuu.


Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.


Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu, na mimi ndani yake.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


Na itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo watakwitwa wana wa Mungu aliye hayi.


Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.


Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;


mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;


katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.


Kristo akae mioyoni mwemi kwa imani; illi ninyi, mkiwa na mizizi na misingi katika upendo,


Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.


Ilinde ile amana nzuri kwa Rolio Mtakatifu akaae ndani yetu.


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.


Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema burre? Roho ikaayo ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu?


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Killa aungamae ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, nae ndani ya Mungu.


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wana Adamu, nae atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Mungu wao.


Yeye ashindae atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, nae atakuwa Mwana wangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo