Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 6:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 6:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali!


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.


NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;


Siibatili neema ya Munga. Maana, ikiwa haki hupatikana kwa sharia, bassi, Kristo alikufa burre.


Mmepatikana na mateso makubwa namna hii burre? ikiwa ni burre.


Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida.


Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana;


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.


killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo