Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 5:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kupitia kwa Isa Al-Masihi, na kutupatia sisi huduma ya upatanisho:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Haya yote yanatokana na Mwenyezi Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Isa Al-Masihi na kutupata sisi huduma ya upatanisho:

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 5:18
29 Marejeleo ya Msalaba  

Na nyumba yo yote mwingiayo, kwanza neneni, Amani iwe nyumbani humu.


na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akikhubiri amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Maana kama vile mwanamke alitoka katika mwanamume, vivyo hivyo mwanamume nae huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu.


pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu yule yule azitendae kazi zote katika wote.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


illakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu, aliye Baba, ambae vitu vyote vimetokana nae, na sisi twarejea kwake; na yuko Bwana mmoja Yesu Kristo, ambae kwa sabiki yake vitu vyote vimekuwa, na sisi kwa sabiki yake.


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.


Hili ndilo pendo, si kwamba sisi twalimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akampeleka Mwana wake kuwa kipatanislio kwa dhambi zetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo