Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 5:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 tena alikufa kwa ajili ya wote, illi walio hayi wasiwe hayi kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuliwa kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuliwa kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuliwa kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 5:15
41 Marejeleo ya Msalaba  

Ya kwamba atatupa sisi, tukiokoka mikononi mwa adui zetu, tumwabudu pasipo khofu,


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu.


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.


Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?


tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu u katika hali ya kufa kwa sababu ya dhambi, bali roho yenu i katika hali ya uzima, kwa sababu ya haki.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya roho ni uzima na amani.


vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, bali faida yao walio wengi, wapafe kuokolewa.


Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena.


Tukiisbi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza.


mkizikwa pamoja nae katikti ubatizo, katika huo mlifufuliwa pamoja nae, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.


BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wana Adamu,


aliyekufa kwa ajili vetu, illi tuishi pamoja nae, ikiwa twakesha au ikiwa twalala.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


Maana kwa ajili hiyo na wao waliokufa walikhubiriwa Injili, illi waluikumiwe katika mwili wahukumiwavyo wana Adamu; bali wawe hayi katika roho kwa kumtii Mungu.


Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo