Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 5:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Maana hatujisifu nafsi zetu mbele yenu marra ya pili, bali tukiwapeni sababu ya kujisifu kwa ajili yetu, illi mpate kuwa nayo mbele yao wanaojisifu kwa mambo ya nje tu, wala si kwa mambo ya moyoni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka kuwapa nyinyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka kuwapa nyinyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka kuwapa nyinyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu, mweze kuwajibu hao wanaoona fahari kuhusu mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 5:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.


Maana hatuthubutu kujihesabu pamoja nao wenye kujisifu nafsi zao, wala kujilinganisha nao: bali wao wakijipima nafsi zao na nafsi zao na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.


Maana mtu mwenye kubaliwa si yeye ajisifuye, hali yeve asifiwae na Bwana.


Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.


Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga ninyi wala si kuwaangusha), sitatahayarika;


Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu, nijapokuwa si kitu.


JE! tunaanza tena kujisifu nafsi zetu? au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa zetu kwenu, au zitokazo kwenu?


bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,


kujisifu kwenu kupate kuzidi katika Kristo Yesu kwa ajili yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi nyote tena.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo