Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 5:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Basi, sisi tunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyo tunajitahidi kuwavuta watu. Mungu anatujua waziwazi, nami natumaini kwamba nanyi pia mnatujua kinaganaga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Basi, sisi tunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyo tunajitahidi kuwavuta watu. Mungu anatujua waziwazi, nami natumaini kwamba nanyi pia mnatujua kinaganaga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Basi, sisi tunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyo tunajitahidi kuwavuta watu. Mungu anatujua waziwazi, nami natumaini kwamba nanyi pia mnatujua kinaganaga.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Mwenyezi Mungu, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Mwenyezi Mungu, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mwenyezi Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 5:11
39 Marejeleo ya Msalaba  

Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule.


Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa.


Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.


wakisema, Mtu huyu huwavuta watu illi wamwabudu Mungu kinyume cha sharia yetu.


Akatoa hoja zake katika sunagogi killa sabato akawavuta Wayahudi na Wayunani waamini.


Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.


Kwa maana mfalme anajua khabari za mambo haya, na naweza kusema nae bila khofu, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni.


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.


Bassi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anakusihini kwa vinywa vyetu: twawaombeni kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


mkitumikiana katika khofu ya Kristo.


Ni jambo la kutisba kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hayi.


maana Mungu wetu ni moto ulao.


bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili.


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo