Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 5:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapongolewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapongolewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapong'olewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kwa maana twajua kama hema letu la dunia tunayoishi likiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 5:1
25 Marejeleo ya Msalaba  

Sisi twalimsikia akiseina, Mimi nitaivunja hekalu hii iliyofanyika kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga ingine isiyofanyika kwa mikono;


Illakini yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanyika kwa mikono, kama vile asemavyo nabii:


Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.


Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi.


Kwa maana sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, hali kuvikwa vazi jingine, illi kitu kile kipatwacho na mauti kimezwe na uzima.


Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo;


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu.


Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,


Bassi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na ntawa,


Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti.


Hivi tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, na mbele zake tutatuliza mioyo yetu


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo