Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 3:5
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu.


Mimi mzabibu; ninyi matawi; akaae ndani yangu, na mimi ndani yake, huyu huzaa Sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno.


Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,


Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.


Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.


Mimi nilipanda, Apollo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.


Akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Bassi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, illi uweza wa Kristo ukae juu yangu.


katika hao wa kwanza manukato ya mauti yao waendao hatta mauti; katika hao wengine manukato ya uzima wao waendao hatta uzima. Na nani atoshae kwa mambo haya?


Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi.


kwa maana ni Mungu atendae ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa ajili ya kusudi lake jema.


Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu.


Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo