Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 3:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 mnadhihirishwa kuwa m barua ya Kristo iliyo kazi ya khuduma yetu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho ya Mungu aliye hayi; si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Ni dhahiri kwamba nyinyi ni barua ya Kristo aliyoipeleka kwa mikono yetu. Barua yenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; imeandikwa si juu ya kipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Ni dhahiri kwamba nyinyi ni barua ya Kristo aliyoipeleka kwa mikono yetu. Barua yenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; imeandikwa si juu ya kipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Ni dhahiri kwamba nyinyi ni barua ya Kristo aliyoipeleka kwa mikono yetu. Barua yenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; imeandikwa si juu ya kipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua inayotoka kwa Al-Masihi, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Al-Masihi, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mwenyezi Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 3:3
35 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


Bassi, ikiwa khuduma ya mauti katika maandiko, iliyochorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hatta wana wa Israeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao utukufu uliokuwa ukibatilika;


Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,


Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo.


Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Pergamo, andika; Haya ayanena yeye aliye na upanga mkali, mkali kuwili;


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Thuatera andika, Haya ayanena Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho kama mwako wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi.


NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.


Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu.


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo