Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 3:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, unaotoka kwa Bwana Isa, aliye Roho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana Isa, ambaye ndiye Roho.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 3:18
24 Marejeleo ya Msalaba  

Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Maneno hayo aliyasema Isaya alipouona utukufu wake, akataja khabari zake.


Nami, utukufu ule ulionipa nimewajia wao, wawe umoja, kama sisi tulivyo umoja:


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake.


Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, illi awe mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi.


illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.


Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sharia ya Mungu wala haiwezi.


Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.


Na kama tulivyoichukua sura yake wa udongo, kadhalika tulaichukua sura yake wa mbinguni.


Bassi Bwana ndiye Roho huyo; walakini alipo Roho ya Bwana, hapo ndipo panapo uhuru.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.


mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.


kama vile ilivyonenwa katika injili ya utukufu wa Mungu ahimidiwae, niliyoaminiwa mimi.


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


Kwa sababu mtu akiwa msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyu ni kama mtu anaejiangalia uso wake wa asili katika kioo.


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo