Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na neno la Mungu ili tujifaidishe. Bali tunalinena neno lake kwa unyofu katika Al-Masihi tukiwa mbele za Mungu, kama watu waliotumwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Al-Masihi tunalisema Neno la Mungu kwa unyoofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 2:17
30 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba,


Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


bassi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochacha, ndio weupe wa moyo na kweli.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu halikuwa ndiyo na siyo.


Kwa nini? kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.


Mwadhani ya kuwa tunajindhuru kwenu tena? Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na haya yote, wapenzi, kwa ajili ya kuwajenga.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,


Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha hivi upesi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo,


bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.


ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo