Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 2:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Lakini Mungu apewe shukrani, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Al-Masihi. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Lakini Mwenyezi Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Al-Masihi. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 2:14
27 Marejeleo ya Msalaba  

Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


Lakini katika mambo haya yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.


Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, ipendavyo Roho yule yule;


nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, illa punje tupu, ikiwa ya nganu au nyingineyo;


Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


ninyi nanyi mkisaidiana kwa ajili yetu katika kuomba, illi, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa kazi ya watu wengi, watu wengi watoe mashukuru kwa ajili yetu.


Lakini Mungu ashukuriwe atiae bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.


Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo.


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;


Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi; tena nimejaa tele, nimepokea kwa mkono ya Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.


Maana kutoka kwenu Neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu: bali na katika killa mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea, hatta hatuna haja sisi kunena lo lote.


Maana shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu;


Bassi nataka wanaume waombe killa mahali, wakimua mikono mitakatifu, pasipo hasira na majadiliano.


Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.


wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo