Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 2:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Al-Masihi kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Al-Masihi kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 2:10
7 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.


Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia, wamefungiwa.


Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na nweza wa Bwana wetu Yesu Kristo,


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Bassi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anakusihini kwa vinywa vyetu: twawaombeni kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.


katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki,


tena mwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkiachiliana, kama na Mungu katika Kristo alivyowaachilia ninyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo