Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 13:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Maana twafurahi, sisi tulipo dhaifu, na ninyi hodari. Tena twaomba hili nalo, mtimilike.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini nyinyi mna nguvu; kwa hiyo tunaomba mpate kuwa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini nyinyi mna nguvu; kwa hiyo tunaomba mpate kuwa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini nyinyi mna nguvu; kwa hiyo tunaomba mpate kuwa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Tunafurahi wakati wowote tunapokuwa dhaifu, lakini ninyi mkawa na nguvu. Nayo maombi yetu ni kwamba mpate kuwa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Tunafurahi wakati wowote sisi tunapokuwa dhaifu, lakini ninyi mkawa na nguvu. Nayo maombi yetu ni kwamba mpate kuwa wakamilifu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 13:9
21 Marejeleo ya Msalaba  

Killa mtu miongoni mwetu ampendeze jirani yake apate wema akajengwe.


Nawasihi ninyi, ndugu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnene nyote mamoja, pasiwe kwenu faraka, bali mwe mmekhitimu katika nia moja na shauri moja.


Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na khofu na matetemeko mengi.


Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.


Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Bassi hapo mauti hufanya kazi yake ndani yetu, hali nzima ndani yenu.


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


usiku na mchana tukiomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu.


illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.


na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu,


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo