Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 12:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi mbeleni, na wala hawajatubu kwa uchafu wao, uasherati, na ufisadi walioushiriki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi mbeleni, na wala hawajatubu kwa uchafu wao, uasherati, na ufisadi walioushiriki.

Tazama sura Nakili

2 Wakorintho 12:21
37 Marejeleo ya Msalaba  

Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.

ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.

YAKINI khabari imeenea ya kama kwenu kuna zina, na zina hiyo ya namna isiyonenwa hatta katika mataifa, kwamba mtu awe na mke wa baba yake.

tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.

Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi.

Nimetangulia kuwaambia: na kama vile nilipokuwapo marra ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo natangulia kuwaambia wao waliofanya dhambi zamani, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia:

Bassi waonyesheni mbele ya makanisa bayana ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.

Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki,

Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:

Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.

wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:

bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili.

Kama vile bodoma na Gomora, na miji iliyozunguka, waliofuata uasharati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wamepasiwa hukumu yamoto wa milele.

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.

Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.

Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo