Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 12:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Na kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu: ingawa nizidipo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda nyinyi mno?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda nyinyi mno?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda nyinyi mno?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Je, ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Hata ingawa inaonekana ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 12:15
22 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;


vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.


Lakini ikiwa sisi tu katika shidda, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu, ufanyao kazi yake kwa kuvumilia mateso yale yale tuteswayo na sisi: au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu.


Kwa nini? kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.


Tazama hii ni marra ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawidemea. Maana sitafuti vitu vyenu, bali ninyi: maana haiwapasi watoto kuwawekea akiba wazazi, bali wazazi watoto.


Akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Bassi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, illi uweza wa Kristo ukae juu yangu.


Nami naliwaandikia neno lili hili, illi, nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumainia ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.


Bassi hapo mauti hufanya kazi yake ndani yetu, hali nzima ndani yenu.


Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu, hatukumharibu mtu, hatukumkalamkia mtu.


Sisemi neno hili illi niwahukumu ninyi; kwa maana nimetangulia kusema ya kwamba ninyi m katika mioyo yetu mpaka kufa pamoja, na kuishi pamoja.


Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.


Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


Vivyo hivyo sisi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapeni, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.


Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo