Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 12:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Tazama hii ni marra ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawidemea. Maana sitafuti vitu vyenu, bali ninyi: maana haiwapasi watoto kuwawekea akiba wazazi, bali wazazi watoto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni nyinyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni nyinyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni nyinyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Sasa niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Nami sitawalemea, kwa sababu sihitaji chochote chenu, ila ninawahitaji ninyi. Kwa kuwa watoto hawaweki akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi huweka akiba kwa ajili ya watoto wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Sasa niko tayari kuja kwenu kwa mara hii ya tatu, nami sitawalemea, kwa sababu sitahitaji chochote chenu, ila ninawahitaji ninyi, kwa kuwa hata hivyo watoto hawaweki akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi huweka akiba kwa ajili ya watoto wao.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 12:14
28 Marejeleo ya Msalaba  

Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.


Mtu asitafute kujifaidia nafsi yake, bali kumfaidia mwenzake.


vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, bali faida yao walio wengi, wapafe kuokolewa.


mtu akiwa na njaa, ale nyumbani; msipate kukutanika kwa hukumu. Nayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.


Lakini nitakuja kwenu, nikipita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.


Lakini nitakuja kwemi upesi, Bwana akipenda, nami nitajua, si neno lao waliojivuna, bali nguvu zao.


Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.


Bassi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nikhubiripo, nitatoa Injili ya Kristo bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu haki yangu niliyo nayo katika Injili.


Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, illi nipate watu wengi zaidi.


Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili;


Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda.


Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, illa kwa kuwa mimi sikuwalemea. Mnisamehe udhalimu huo.


Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.


BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


vile vile kama mjuavyo jinsi tulivyomwonya killa mmoja wemi kama baba amwonavyo mtoto wake, tukiwatieni moyo na kushuhudia,


Vivyo hivyo sisi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapeni, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo