Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 12:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu, nijapokuwa si kitu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Nimekuwa kama mpumbavu, lakini nyinyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Nyinyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Nimekuwa kama mpumbavu, lakini nyinyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Nyinyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Nimekuwa kama mpumbavu, lakini nyinyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Nyinyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Nimejifanya mjinga, lakini mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora”, ingawa mimi si kitu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Nimekuwa mjinga, lakini ninyi mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora,” ingawa mimi si kitu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 12:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kadhalika na ninyi, mkiisha kufanya vyote mlivyoamriwa, semeni, Sisi watumishi wasiofaa; tumetenda yaliyotupasa kutenda.


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.


Kwa maana vyote ni vyenu; ikiwa ni Paolo, au Apollo, au Kefa, au dunia, au uzima, au mauti, au vile vilivyo sasa, au vile vitakavyokuwa,


Lakini ikiwa sisi tu katika shidda, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu, ufanyao kazi yake kwa kuvumilia mateso yale yale tuteswayo na sisi: au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokofu wenu.


INGEKUWA kheri kama mngenisamehe kidogo upumbavu wangu; naam, kanisameheni.


Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa kitu walicho nacho mitume walio wakuu.


Maana ishara za mtume zilitendwa kati yenu katika uvumilivu wote, kwa ishara na maajabu na nguvu.


Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini nitajizuia, mtu asinihesabie zaidi ya haya ayaonayo kwangu au kuyasikiakwa kinywa changu.


JE! tunaanza tena kujisifu nafsi zetu? au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa zetu kwenu, au zitokazo kwenu?


Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.


Maana mtu akijiona kuwa kitu, nae si kitu, ajidanganya nafsi yake.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo