Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 12:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 SINA buddi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia njozi na mafunuo ya Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono na ufunuo alivyonijalia Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono na ufunuo alivyonijalia Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono na ufunuo alivyonijalia Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Yanipasa nijisifu. Ingawa haifaidi kitu, nitanena kuhusu maono na mafunuo kutoka kwa Bwana Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Yanipasa nijisifu, ingawa haifaidi kitu. Nitaenda kwenye maono na ufunuo kutoka kwa Bwana Isa.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 12:1
26 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu.


Na Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi shauri kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.


Bwana akamwambia Paolo kwa njozi nsiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Vitu vyote ni halali kwangu; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali kwangu; hali si vitu vyote vijengavyo.


Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho?


Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.


Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu, nijapokuwa si kitu.


Kwa khabari za mtu huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika khabari ya udhaifu wangu.


Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi.


Akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Bassi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, illi uweza wa Kristo ukae juu yangu.


Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, wapata mwaka, licha ya kutenda hivi, hatta kutaka pia.


Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.


Nami nalikwenda kwa kufunuliwa, nikawaeleza injili ile niikhubirivyo katika mataifa, lakini kwa faraglia kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio burre au nalipiga mbio burre.


ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,


Maana twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hayi, tutakaosalia hatta wakati wa kuja kwake Bwana, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo