Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 11:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Je! nalifanya dhambi kwa kujinyenyekea illi ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwakhubiri Injili ya Kristo bila ujira?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo?

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 11:7
14 Marejeleo ya Msalaba  

Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.


Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono hii imetumika kwa mahitaji yangu na yao walio pamoja nami.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.


Au je! ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo kutokufanya kazi?


NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;


na kupata ziada hatta kuikhuhiri Injili katika inchi zilizo mpaka mmoja na inchi zenu; tusijisifu katika cheo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.


Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, illa kwa kuwa mimi sikuwalemea. Mnisamehe udhalimu huo.


Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,


Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu.


wala hatukula chakula kwa mtu ye yote burre, bali kwa taabu na masumbufu, mchana na usiku, tulitenda kazi, illi tusimlemee mtu kwenu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo