Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 11:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo killa siku, ndio maangalizi ya makanisa yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa kila siku na mzigo wa wajibu wangu kwa makundi yote ya waumini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa na mzigo wa wajibu wangu kwa makundi yote ya waumini.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 11:28
12 Marejeleo ya Msalaba  

Baada ya siku kadha wa kadha Paolo akamwambia Barnaba, Haya! turejee sasa tukawaangalie ndugu katika killa mji tulipolikhubiri neno la Bwana, wa hali gani.


Hatta akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya inchi ya Galatia na Frugia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.


Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.


Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Nawiwa na Wayunani na washenzi, nawiwa na wenye hekima na wajinga.


Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu.


illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


waliokuwa tayari hatta kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, illa na makanisa ya mataifa yote pia;


Lakini Mungu alivyomgawia killa mtu—kama Mungu alivyomwita killa mtu, na aenende vivyo hivyo. Na ndivyo ninavyoagiza katika Makanisa yote.


MAANA nataka muijue juhudi niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili, jinsi ilivyo kuu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo