Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 11:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 kwa kusafiri marra nyingi; khatari za mito; khatari za wanyangʼanyi; khatari kwa jamaa; khatari kwa mataifa; khatari za mijini; khatari za jangwani; khatari za baharini; khatari kwa ndugu za uwongo;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 nimekuwa katika safari za mara kwa mara. Nimekabiliwa na hatari za kwenye mito, hatari za wanyang’anyi, hatari kutoka kwa Wayahudi wenzangu, hatari kutoka kwa watu wa Mataifa; hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini; na hatari kutoka kwa ndugu wa uongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 katika safari za mara kwa mara. Nimekabiliwa na hatari za kwenye mito, hatari za wanyang’anyi, hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, hatari kutoka kwa watu wa Mataifa; hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini; na hatari kutoka kwa ndugu wa uongo.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 11:26
35 Marejeleo ya Msalaba  

Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.


Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe,


Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.


Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.


Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;


Hatta Gallio alipokuwa Prokonsuli wa Akaya, Wayahudi wakamwendea Paolo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu,


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile.


nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi;


Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, Wayahudi wakamfanyyia vitimbi, alipotaka kwenda Sham kwa njia ya bahari: bassi akaazimu kurejea kwa ujia ya Makedonia.


Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paolo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumpokonya mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.


na kumwomba awafadhili, na kutoa amri aletwe Yerusalemi, wapate kumwotea na kumwua njiani.


Shauri la askari lilikuwa wafungwa wauawe, mtu asiogelee na kukimbia.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


Ni nani atakaetutenga na upendo wa Kristo, Je! ni shidda, au dhiiki, au adha, au njaa, au uchi, au khatari, au upanga?


Kwa nini wakabatizwa kwa ajili yao? Na sisi, kwa nini tumo khatarini killa saa?


Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.


Katika Dameski liwali wa Areta mfalme alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, akitaka kunikamata;


bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo