Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 11:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Wao wakhudumu wa Kristo? (nanena kiwazimu), mimi zaidi; kwa kazi kuzidi sana; kwa mapigo kupita kiasi; kwa vifungo kuzidi sana; kwa mauti marra nyingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi – nanena hayo kiwazimu – ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi – nanena hayo kiwazimu – ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi — nanena hayo kiwazimu — ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Je, wao ni watumishi wa Al-Masihi? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii zaidi yao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimepigwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Je, wao ni watumishi wa Al-Masihi? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii kuwaliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 11:23
43 Marejeleo ya Msalaba  

Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.


illa ya kuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na mateso yaningoja.


Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paolo akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa mataifa.


Na walipokuwa wakikaa huko siku nyingi, Festo akamweleza mfalme khabari za Paolo, akisema, Yupo hapa mtu aliyeachwa na Feliki kifungoni;


BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.


Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.


Paolo akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akikhubiri khabari za ufalme wa Mungu, na kuwafundisha watu mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.


Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.


Kama ilivyoandikwa, ya kama, Kwa ajili yako tunauawa mchana kuchwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.


Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


MTU na atubesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.


Hatta saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa makofi, hatuna makao;


Maana nadhani ya ku wa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia na malaika na wana Adamu.


Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.


Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa kitu walicho nacho mitume walio wakuu.


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti.


kama wasiojulika, bali wajulikao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hayi; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;


Tangu sasa mtu asinitie taabu; kwa maana ninachiukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.


KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


kwayo ni mjumbe kifungoni; nipate ujasiri katika kunena jinsi nipaswavyo kusema.


hatta vifungo vyaugu vimekuwa dhahiri katika Kristo, katika praitorio, na kwa wengine wote.


Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


nami najitaabisha kwa hiyo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendae kazi ndani yangu kwa nguvu.


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata.


Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;


Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.


illakini, kwa ajili ya upendo, nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paolo mzee, na sasa mfungwa wa. Yesu Krlsto pia.


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo