Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 11:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Bassi si neno kubwa wakhudumu wake nao wakijigeuza wawe mfano wa wakhudumu wa haki. Mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa hiyo basi si ajabu kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 11:15
30 Marejeleo ya Msalaba  

Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?


atakaemlipa killa mtu kwa kadiri ya matendo yake;


Kwa maana tusiseme (kama tulivyosingiziwa nakama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba sisi twanena), Na tufanye mabaya, illa yaje mema? kuhukumiwa kwao kuna haki.


Ikiwa sisi twaliwapandieni vitu vya rohoni, je! ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?


Maana hawo ni mitume wa uwongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume ya Kristo.


Wao wakhudumu wa Kristo? (nanena kiwazimu), mimi zaidi; kwa kazi kuzidi sana; kwa mapigo kupita kiasi; kwa vifungo kuzidi sana; kwa mauti marra nyingi.


Kwa maana ikiwa khuduma ya hukumu ina utukufu, khuduma ya haki ina utukufu unaozidi sana.


Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.


Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.


Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.


Na juu yao wana mfalme, malaika wa abuso, jina lake kwa Kiebrania Abaddon, na kwa Kiyunani jina lake Apollion.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo