Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 10:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 10:4
28 Marejeleo ya Msalaba  

Musa akafundishwa hekima yote ya Misri, akawa hodari wa maneno na matendo.


Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.


wala msitoe viungo vyenu kuwa silaha ya dhulumu kwa dhambi; bali jitoeni nafsi zenu sadaka kwa Mungu kama walio hayi baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.


imani yenu isiwe katika hekima ya wana Adamu, bali katika nguvu za Mungu.


Nani aendae vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Nani apandae mizabibu asiokula baadhi ya matunda yake? Au nani achungae kundi, asiyekula haadhi ya maziwa ya kundi?


Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga ninyi wala si kuwaangusha), sitatahayarika;


Kwa biyo, naandika liayo nisipokuwapo, illi, nikiwapo, nisitumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana illi kujenga wala si kubomoa.


si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu,


Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi.


katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,


Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu.


Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri;


Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo.


Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zikiisha kuzungukwa siku saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo