Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 10:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 10:3
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.


kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa: bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.


illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.


Bassi, nilipokusudia haya nalitumia kigeugeu; au niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili illi iwe hivi kwangu, kusema ndiyo, ndiyo, na siyo, siyo?


maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Agizo hilo nakupa iwe akiba, mwanangu Timotheo, kwa ajili ya maneno ya unabii yalivotangulia juu yako, illi katika hayo ufanye vile vita vizuri;


Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


BASSI na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, tuweke kando killa mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa uvumilivu katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo