Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 10:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhani ya kuwasisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nawaomba nitakapokuja kwenu nisipaswe kuwa na ujasiri dhidi ya watu fulani kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata mtazamo wa ulimwengu huu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani, kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 10:2
12 Marejeleo ya Msalaba  

SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.


Kwa maana wale wafuatao mambo ya mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale wafuatao mambo ya roho hufikiri mambo ya roho.


Bassi, nilipokusudia haya nalitumia kigeugeu; au niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili illi iwe hivi kwangu, kusema ndiyo, ndiyo, na siyo, siyo?


Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Illakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), na mimi niuao ujasiri.


Kwa biyo, naandika liayo nisipokuwapo, illi, nikiwapo, nisitumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana illi kujenga wala si kubomoa.


Nimetangulia kuwaambia: na kama vile nilipokuwapo marra ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo natangulia kuwaambia wao waliofanya dhambi zamani, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo