Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 10:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Maana mtu mwenye kubaliwa si yeye ajisifuye, hali yeve asifiwae na Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa na Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa na Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa na Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa maana si yeye ajisifuye mwenyewe akubaliwaye, bali yeye ambaye Mwenyezi Mungu humsifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa maana si yeye ajisifuye mwenyewe akubaliwaye, bali yeye ambaye Mwenyezi Mungu humsifu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 10:18
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.


Kwa maana waliupenda utukufu wa wana Adamu kuliko utukufu wa Mungu.


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu.


Nisalimieni Apelle, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumba ya Aristobulo.


hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu.


kwa maana lazima kuwapo uzushi kwenu, illi waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Maana hatuthubutu kujihesabu pamoja nao wenye kujisifu nafsi zao, wala kujilinganisha nao: bali wao wakijipima nafsi zao na nafsi zao na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.


Na namwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, bali ninyi mfanye lililo jema, tujapokuwa sisi kama waliokataliwa.


JE! tunaanza tena kujisifu nafsi zetu? au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa zetu kwenu, au zitokazo kwenu?


Maana hatujisifu nafsi zetu mbele yenu marra ya pili, bali tukiwapeni sababu ya kujisifu kwa ajili yetu, illi mpate kuwa nayo mbele yao wanaojisifu kwa mambo ya nje tu, wala si kwa mambo ya moyoni.


bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,


Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.


illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo