Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 1:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na nyinyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na nyinyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na nyinyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Al-Masihi. Alitupaka mafuta

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Al-Masihi. Ametutia mafuta

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 1:21
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.


Bassi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lili hili ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho.


mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;


Lakini Bwana ni mwaminifu, atakaewafanyeni imara na kuwaokoeni na yule mwovu.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.


Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo