Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 1:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Al-Masihi ni “Ndiyo”. Kwa sababu hii, ni kwake yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Al-Masihi ni “Ndiyo.” Kwa sababu hii ni kwake yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 1:20
41 Marejeleo ya Msalaba  

Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika daraja ya mjinga ataitikaje, Amin, baada ya kushukuru kwako, nae hayajui usemayo?


Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele.


Bali yeye, ambae uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.


Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia.


Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwana wake.


Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu.


wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo