Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 1:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 ninyi nanyi mkisaidiana kwa ajili yetu katika kuomba, illi, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa kazi ya watu wengi, watu wengi watoe mashukuru kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 nyinyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 nyinyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 nyinyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 kama vile mnavyoungana kusaidiana nasi katika maombi. Hivyo wengi watatoa shukrani kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka za neema tulizopata kwa majibu ya maombi ya wengi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kama vile mlivyoungana kusaidiana nasi katika maombi, hivyo wengi watatoa shukrani kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka za neema tulizopata kwa majibu ya maombi ya wengi.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 1:11
15 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi Petro akalindwa gerezani, sala zikawa zinafanyika kwa juhudi sana na Kanisa mbele za Mungu kwa ajili yake.


Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe.


Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu.


Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokofu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho ya Yesu Kristo,


mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,


ILIYOBAKI, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, likatunzwe vilevile kama ilivyo kwenu;


Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.


Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo