Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 4:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Bali wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 4:5
28 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi yule aliyepokea talanta tano akashika njia, akafanya kazi nazo, akachuma talanta nyingine tano.


Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe.


Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia Wote, Kesheni.


Wa kheri watumishi wale ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesba. Amin, nawaambieni, atajifunga, atawaketisha, atakuja kuwakhudumia.


Assubuhi yake sisi tulifuatana na Paolo tukatoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, Mwinjilisti, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


ambalo nimekuwa mkhudumu wake, kwa uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu;


Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize.


Bassi tusilale kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.


Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu.


Uyatafakari hayo, ukae katika hayo. Kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.


Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;


Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.


Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo.


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe manibo yaliyosalia, yaliyo tayari kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo