Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 4:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu watakaowaambia yale masikio yao yanatamani kusikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 4:3
33 Marejeleo ya Msalaba  

Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata saa hiyo hiyo, wakawaogopa watu: maana walitambua ya kuwa ule mfano amewanena wao.


Ole wenu ninyi, wana Adamu wote watakapowanena vema: maana baba zao waliwatenda manabii ya uwongo mambo kamsi hayo.


Nami, kwa sababu naisema kweli, hamniamini.


Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana faragha kwa neno lo lote illa kutoa khabari na kusikiliza khabari za jambo jipya.


NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.


Na neno langu na kukhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya kibinadamu yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho zenye nguvu,


Bassi, je! nimekuwa adui wenu kwa sababu nawa ambieni yaliyo kweli?


na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;


Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu.


ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo