Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 3:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Killa andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibu katika haki;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Maandiko yote yamevuviwa na Mungu, na yafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kila Andiko limevuviwa na Mwenyezi Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki,

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 3:16
43 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.


Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?


Akawaambia, Imekuwaje bassi Daud katika Roho kumwita Bwana, akinena,


Yatatimizwaje bassi maandiko, kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kuwa?


Lakini jambo hili lote limekuwa, illi maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.


Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hamjidanganyi kwa sababu hii, kwa kuwa bamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?


Kwa sababu Daud mwenyewe alisema, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako.


Ikiwa aliwaita wale miungu waliojiliwa na neno la Mungu (na maandiko hayawezi kutanguka),


Maana killa atendae manyonge huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasikemewe;


Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,


Mtu huyu alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikiwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi khabari za Bwana; nae alijua ubatizo wa Yohana tu.


ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba,


Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


Na walipokuwa hawapatani wao kwawao, wakaenda zao, Paolo alipokwisha kusema neno hili moja ya kama, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,


Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.


mkufunzi wra wajiuga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati,


Kwafaa sana kwa killa njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.


Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake,


Lakini killa mmoja hupewa ufunuo wa Roho illi kufaidia.


Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.


akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.


Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake,


Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo