Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 3:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 na jinsi tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kupitia kwa imani katika Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 3:15
38 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajihu, akawaamhia, Mwajidanganya, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.


Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Mtoto yule akakua, akaongezeka nguvu, akajazwa hekima; neema ya Mungu ikawa pamoja nae.


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwa ikiwaka ndani yetu, alipokuwa akisema nasi njiani, akitufunulia maandiko?


Ndipo akaamsha akili zao, wapate kuyatambua maandiko matakatifu.


Illakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaaminije maneno yangu?


Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi.


Hatta walipomaliza yote aliyoandikiwa, wakamshusha katika mti, wakamweka kaburini.


AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.


Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu,


Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa sauti kuu, Paolo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugenza akili zako.


ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


Na ninyi, akina baba, msiwachokoze watoto wemi; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.


Hatta nijapo, fanya bidii katika kusoma na kuonya ua kufundisha.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo:


nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo.


vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa khabari za mambo hayo mumo humo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa upotevu wao wenyewe.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo