Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 2:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Yafahamu sana hayo nisemayo, maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Mwenyezi Mungu atakupa ufahamu katika mambo haya yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo hayo yote.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 2:7
40 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


Ndipo akaamsha akili zao, wapate kuyatambua maandiko matakatifu.


Yawekeni maneno haya masikioni mwenu: kwa maana Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


akamtoa katika misiba yake yote, akampa kibali na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri: nae akamfanya msimamizi wa Misri na nyumba yake yote.


Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, ipendavyo Roho yule yule;


Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


Uyatafakari hayo, ukae katika hayo. Kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.


Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kuyashiriki matunda.


Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daud, kama inenavyo injili yangu.


Maana mtafakarini sana yeye aliyeyavumilia mapingamizi makuu namna hii ya wenye dhambi juu ya nafsi zao, msije mkadhoofika mkizimia mioyoni mwenu.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Bassi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambae Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya maleka yaliyo mema.


Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa.


Hekima hii siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na ya Shetani,


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo