Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 2:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Tena haimpasi mtumishi wa Bwana Isa kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Tena haimpasi mtumishi wa Bwana Isa kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 2:24
31 Marejeleo ya Msalaba  

Hatateta, wala hatapaaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.


Bassi Wayahudi wakashindana wao kwa wao, wakinena; Awezaje mtu huyu kutupa sisi nyama yake tuile?


Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.


Pakawa makelele mengi. Waandishi wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakamtetea, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema nae tusishindane na Mungu.


Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi m ndugu: Mbona mnadhulumiana?


NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;


maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;


bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano;


Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano,


Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;


mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi.


bali tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa,


Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu,


alishikae neno la imani kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupingana nae.


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


Mwatamani, wala hanma kitu; mwana na kuona wivu, na hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi.


Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo