Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 2:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa unajua hayo huzaa magomvi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 2:23
7 Marejeleo ya Msalaba  

wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo.


Bali hadithi za kizee, zisizo za dini, uzikatae.


Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.


Jiepushe na maneno yasiyo na maana, yasiyo ya dini; maana wataendelea zaidi katika maovu;


Maswali ya upuzi, na vitabu vya nasaba, na magomvi, na mashindano ya sharia, ujiepushe nayo. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.


VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo