Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Timotheo 2:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Bassi katika nyumba havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina heshima.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: Vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: Vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida.

Tazama sura Nakili

2 Timotheo 2:20
15 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu.

La! si hivyo, ee bin-Adamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Ya nini nkanifanza hivi?

Maana ninyi mwafanya kazi pamoja na Mungu: ninyi m shamba la Mungu, m jengo la Mungu.

Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi.

katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.

ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo