Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 2:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Mwenyezi Mungu anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Mwenyezi Mungu na auache uovu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Lakini msingi wa Mwenyezi Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana Mwenyezi anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Bwana Mwenyezi, na auache uovu.”

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 2:19
69 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwafahamu ninyi wakati wo wote: ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa katika mwamba.


Akawaambia, Ya nani sanamu hii na anwani hii?


kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.


nae atasema, Nawaambieni, Siwajui mtokako: ondokeni mbali nami, ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.


Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba.


Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema; na walio wangu nawajua, na walio wangu wananijua,


Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.


Aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri yake kwamba Mungu ni kweli.


Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia.


Illi wana Adamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao: Asema Bwana afanyae mambo haya yote.


hatta hapa ana mamlaka kwa makuhani wakuu awafunge wote wakuitiao Jina lako.


Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea asili. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele ya Mungu,


Pendo niwe nalo pasipo unafiki; mkichukia lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.


kadhalika nikijitahidi kuikhubiri Injili, nisikhubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine,


nao Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa sababu hii nitakusifu katika Mataifa, Na jina lako nitaliimba.


Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.


kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejuliwa nae.


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Bali sasa, mkiisha kumjua Mungu, ya nini kurejea tena kwa mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge na yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena.


mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;


ambae kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unakwitwa,


Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.


Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo.


Na watumishi wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake katika vipaji vya nyuso zao.


Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo